Jumatatu 29 Desemba 2025 - 23:00
Kitabu cha Al-Ghadir kimeondosha uwezekano wa kukanusha Wilayah ya Amirul-Mu’minin Ali (a.s.)

Hawza/ Hujjatul-Islam Khorrami-Arani, akirejelea kitabu “Al-Ghadir” cha Allama Amini, amekitaja kuwa ni kazi ya kipekee isiyo na mfano na ngome imara mbele ya upotoshaji wa historia.

Hujjatul-Islam Hassan Agha Khorrami-Arani, katika mazungumzo na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza mjini Sari Iran, huku akigusia kuwadia kwa maadhimisho ya kuzaliwa Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) na umuhimu wa kufafanua nafasi yake ya kihistoria na kiitikadi, alisema: Mkusanyiko mkubwa wa juzuu nyingi wa “Al-Ghadir” ulioandikwa na Allama Amini ni urithi wa kielimu wa kudumu, uliotungwa kwa lengo la kutetea kudhulumiwa kwa Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) na kuthibitisha ukhalifa wake baada ya Mtume (s.a.w.). Jambo la kuzingatiwa ni kwamba vyanzo na marejeo yote yaliyotumiwa katika kitabu hiki yamechaguliwa kutoka katika vitabu vya wanazuoni wa Ahlus-Sunna.

Mwalimu wa Hawza, akirejelea upekee wa juhudi na utafiti wa  Allama Amini, alibainisha: Marehemu Allama Amini kwa ajili ya kuandaa kazi hii kubwa, alikuwa akitumia takribani saa 17 kwa siku katika kusoma na kufanya utafiti, na katika mchakato huu alisoma takribani vitabu 10,000 kuanzia mwanzo hadi mwisho, na akarejea zaidi ya vitabu 100,000 mara nyingi. Athari ya ajabu ya kitabu hiki imefikia kiwango ambacho inasimuliwa kuwa baada ya kuchapishwa kwa juzuu moja tu nchini Lebanon, idadi kubwa ya ndugu wa Kisunni, kutokana na hoja zake thabiti na ushahidi wake wa wazi, waliingia katika madhehebu ya haki ya Ushia.

Hujjatul-Islam Khorrami-Arani aligusia muundo na ukubwa wa mkusanyiko huu na akaongeza: Mkusanyiko wa kipekee wa Al-Ghadir katika mpango wake wa awali una juzuu 20, ambapo hadi sasa juzuu 11 zimechapishwa na juzuu 9 nyingine bado hazijachapishwa. Allama Amini mwenyewe alisisitiza kwamba mada kuu na za msingi zimo katika hizo juzuu 9, na hizi juzuu 11 zilizopo ni kama utangulizi wa mijadala hiyo ya kina. Alikuwa na imani kwamba kama mkusanyiko huu ungechapishwa kwa ukamilifu, ungekuwa na athari kubwa sana katika ulimwengu wa Kiislamu.

Akiwa amesisitiza uimara na uthabiti wa kielimu wa kitabu "Al-Ghadir", alisema: Maudhui ya kitabu hiki, japokuwa huenda yasipendeze kwa baadhi ya makundi, lakini kutokana na kutegemea vyanzo imara na vinavyoaminika, katika kipindi cha takribani miaka sitini tangu kichapishwe, hakuna mtu wala kundi lililoweza hata kukosoa au kukanusha kitaalamu hata ukurasa wake mmoja. Kazi hii, pamoja na kukubaliwa na wanazuoni wa Kishia, imepata pia uangalizi na sifa kutoka kwa wanazuoni wakubwa, mafaqihi, wanahadithi na hata watu mashuhuri wa kisiasa wa Ahlus-Sunna, na pongezi nyingi zimeandikwa juu yake.

Mwalimu huyu wa Hawza alisisitiza: Allama Amini kwa kuandika Al-Ghadir, amefunga kabisa njia ya aina yoyote ya kukanusha au kutoa visingizio dhidi ya Hadithi ya Ghadir na Wilayah ya Amirul-Mu’minin Ali (a.s.), na amewasimamishia hoja watu wote. Katika kitabu hiki, amenukuu na kuwasilisha riwaya ya Ghadir kutoka kwa Masahaba 110 wa Mtume (s.a.w.), Tabi‘in 84, na wapokezi 360 kutoka katika vitabu vya Ahlus-Sunna, katika kipindi cha karne ya pili hadi ya kumi na nne Hijria. Wingi huu wa ushahidi unathibitisha kwa uwazi kabisa tawaturi ya Hadithi ya Ghadir.

Hujjatul-Islam Khorrami-Arani aliongeza: Allama Amini alikuwa akisisitiza kwamba, Siku ya Kiyama atanakishiana na maadui wa Amirul-Mu’minin Ali (a.s.), kwa kuwa walimnyima muda wake; na lau si hivyo, angeelekeza juhudi zake kwenye kusambaza maarifa safi ya ‘Alawi, si tu kuthibitisha Imama. Kwa hakika, Allama Amini ni shakhsia iliyosimama peke yake mbele ya wapotoshaji wa historia na kwa kalamu yenye nguvu, mantiki thabiti na msisimko, alielezea haki zilizofichwa katika tabaka za giza za kihistoria, na akauthibitishia ulimwengu ukhalifa wa moja kwa moja wa Imam Ali (a.s.).

Mwisho, akirejelea Hadithi ya Ghadir: “مَنْ كُنْتُ مَوْلَاهُ فَهَذَا عَلِيٌّ مَوْلَاهُ”, alisisitiza nafasi ya msingi ya tukio hili katika kufafanua ufuasi na uhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha